0

WAANDISHI MAFUNZONI

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA




Waandishi wa Habari mkoani Mara wametakiwa kuzingatia maadili ya uandishi wa Habari ili kuepuka matatizo pale wanapoandika na kutoa Habari katika vyombo vyao vya Habari.

Kauli hiyo imetolewa hii leo na Mwezeshaji wa warsha ya maadili ya Uandishi wa Habari na azimio la Dar es salaam kuhusu Uhuru na uwajibikaji  wa vyombo vya Habari Juma Thomas katika ukumbi wa Hotel ya Orange Tree Mjini Musoma.

Amesema ili kuepuka matatizo katika ofikishaji wa Habari,Mwandishi wa Habari anapaswa kufuata maadili yote yanayotakiwa kabla ya kutoa Habari katika chombo cha Habari anachokifanyia kazi.

Thomas amedai kukosekana kwa maadili kwa Waandishi wa Habari kunaweza kupelekea Mwandishi kuandika Habari ambayo haina maadili na ndfipo kunakopelekea Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuandaa kwa warsha za namna hiyo mara kwa mara.

Aidha muwezeshaji huyo ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya Habari kuhakikisha inajali na kubolesha maslahi ya Waandishi wa Habari inaowatumia ili kuweza kuandika na kutoa Habari kwa kufuata maadili na weledi wa kazi ya Uandishi wa Habari.

Akizungumzia azimio la Dar es salaam juu ya Uhuru na Uwajibikaji wa vyombo vya Habari amesema Wanahabari amesema Wanahabari wote wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia ukweli,uadilifu,umahili na weledipamoja na umakini na uwajibikaji wa hali ya juu kwa Umma ili kujenga imani na uaminifu machoni kwa Umma.

Amesema Wanahabari wanapaswa kujenga umoja wa kijamii,kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni kwa kukuza uvumilivu wa tofauti za maoni na imani. 

Post a Comment