MWANDISHI WA HABARI "KULA SHAVU" UJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TAIFA CCM
-Katibu wa CCM atoa onyo kali kwa watakaopiga kampeni
-Asema rushwa ni adui wa haki wawaache wanachama wawachague kutokana na uwezo wao.
Butiama
JINA la Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru na Mzalendo Wilaya ya
Musoma Mkoa wa Mara Eva-Sweet Musiba limeteuliwa kuwa miongoni mwa
wagombea nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Katibu wa CCM
Wilaya ya Butiama, Mercy Mollel alisema kuwa majina hayo yamepitishwa na
ngazi ya Mkoa huku yakisubiri uchaguzi katika mkutano Mkuu wa CCM
wilaya hiyo ambao utafanyika septemba 29 mwaka huu.
Alisema
kuwa zoezi la uchukuaji na urudishaji wa fomu ulishafanyika kwa
mafanikio makubwa ambapo wanachama wengi walijitokeza kuchukua fomu ili
kuwania nafasi mbalimbali katika chama hicho.
Alisema kuwa
taarifa hiyo ya kutangaza majina ya wagombea ni wao kujijua kuwa
wameteuliwa lakini si ruhusa kupiga kampeni hadi pale watati utakapofika
wa kupigiwa kura kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa huo.
Mollel alitoa onyo kali kwa mgombea yeyote atakayepiga kampeni kwa
wanachama kwani akigundulika hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi
ya mgombea huo.
Alitoa wito kwa wagombea hao kufuata kanuni na
taratibu za uchaguzi na kuwaacha wanachama kuwachagua kutokana na uwezo
wao na sio fedha kwani katiba ya chama hicho.
“Katiba yetu
inasema kuwa sitopokea wala kutoa rushwa hivyo natoa wito kwa wagombea
wote wa nafasi mbalimbali waache wanachama wawachague kutokana na uwezo
wao sio kutumia fedha zao kwa kutoa rushwa,”alisema Mollel.
Mollel alizitaja nafasi zilizotolewa ambazo zinawaniwa ni pamoja na
Katibu wa siasa na uwenezi na majina yaliyorudi ni Bwire Gibuma, Ntobi
Ntobi, Japhet Werema, Nafasi ya Katibu wa uchumi na fedha ni Baraka
Imani, Aron Mnema, Magina Nyauko, Nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri ya
Wilaya kundi la Wanawake ni Tabitha Idd, Wegesa Witimu, Mwajuma Magoti
na Bhoke Ngurube.
Nafasi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa
ni Wegesa Witimu, Break Chisumo, Yohana Mnema, Rudia Mazera, Nestor
Matiko na Happiness Masagara. Nafasi ya kundi la wazazi ni Fidelis
Igonge, Wambura Kishamuri, Heonyo M. Heonyo, John Nyamisana, Ibrahim
Makanya na Jemsi Matongo.
Nafasi nyingine ni wajumbe wa Mkutano
Mkuu wa CCM Mkoa ni Nyaget Adam, Joseph Chief, Brasius Chuma, Fidelis
Igonge, Gerald Kasonyi, Sebastian Makakila, Rashid Makka, Jerome
Massawe, Eva-Sweet Musiba wengine ni Vivian Juma, Nyabukika B.
Nyabukika, Magige Nyerere, Bhoke Ngurube, Rosemary Olinda na Wegesa
Witimu.
Alisema kuwa nafasi ya Halmashauri Kuu vijana haikuweza
kutoa wateuliwa kwa kuwa walioomba wote walikuwa na umri mkubwa hivyo
kukosa sifa lakini tayari wameshazitangaza upya na watu wameshachukukua
fomu na wiki mbili zijazo majina yatatolewa.
Aliongeza kuwa kwa
sasa wanasubiria majina ya Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo na wajumbe wa
Halmashauri Kuu CCM Taifa kupitia Wilaya wanasubiria kutoka katika kikao
cha Halmashauri kuu CCM Taifa
Post a Comment
0 comments