0
MGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA


SANYA
Mmoja kati ya Wanachama sita wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mara Sanya Christopher alisema atahakikisha analeta mabadiliko makubwa yakiwemo ya kuchumi ndani ya Chama hicho iwapo vikao vya uteuzi vitampitisha na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kumchagua kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoani Mara.

Akizungumza katika mahojiano na Blogu hii kuhusiana na maamuzi yake ya kuamua kuomba nafasi hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho kuna changamoto nyingi za kwa kiongozi wa Chama,Sanya alisema hilo ameliona na halitampa tabu kwna kuwa amesomea masuala ya uongozi na namna ya kukabiliana na changamoto kama kiongozi.

Alisema licha ya mambo ya nje ya Chama na changamoto zake hali iliyopo ndai ya Chama hicho kwa sasa itampasa pale atakapopata nafasi hiyo kuanza na kuanzisha madarasa ya itikadi kwa makatibu wenezi kuanzia ngazi ya shina hadi Mkoa ikiwa ni kipaumbele cha kwanza kwake ili waweze kukieneza Chama hicho zaidi na kurudisha imani kwa Wanachama na Wananchi.

Sanya alisema ni muhimu kutolewa kwa elimu ya Chama kwa Wanachama ili kila mmoja aweze kuelewa umuhimu wake ndani ya Chama na kutekeleza majukumu yanayompasa katika kukitumikia na kujitambua.

Alisema wapo wagombea ambao wanaomba nafasi kwa ajili ya kutafuta majina na umaarufu na kushindwa kuzitumia kwa kuleta ufanisi na mabadiliko ndani ya Chama hicho na kufanya kuyumba kwa Wanachama huku wengine wakikimbilia katika vyama vya upinzani.

Alisema ni vyema Mwanachama unapoomba nafasi ya uongozi kujiuliza nini utakifanyia Chama kuliko kuomba nafasi kwa kutafuta ufahamike na kuhudhuria vikao bila kuwa na mipango ya kujua namna ya kuongeza Wanachama na kuwajenga kiimani Wanachama wote ili kuepuka mkanganyiko.

Akizungumzia masuala ya kiuchumi,mgombea huyo ambaye ana dhamila ya kuleta mabadiliko makubwa kwa mujibu wa maelezo yake alisema kutokana na vitega uchumi vilivyopo ndani ya Chama hicho haiwezikani Wanachama wake pamoja na viongozi wakashindwa kuendesha vikao vya kujenga Chama kwa kukosa fedha.

Alidai kutokana na vitega uchumi hivyo atahakikisha anasimamia akiwa kama mwana uchumi ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi ndani ya Chama cha Mapinduzi na kila mmoja aweze kuvutiwa na Chama hicho si kwa sera peke yake bali na kujiendesha kiuchumi.

Sanya Christopher anaomba nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapindui Mkoani Mara akiwa ni kada wa Chama hicho ambaye amepitia katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama hicho.
 









 

Post a Comment