MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA |
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara Christopher Sanya amemshukuru Mwenyekiti wa
Chama hicho Taifa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na wajumbe wote waliopitisha
jina lake katika kuwania nafasi hiyo kwa kuwa wamemuamini na kuona anafaa
kukiongoza Chama hicho.
Akizungumza na blogu hii mara baada
ya kikao cha Kamati kuu ya Chama hicho kulitangaza jina lake kuwa mmoja wa
wagombea wa nafasi hiyo katika Mkoa wa Mara,Sanya alisema kazi imebakia kwa
wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa ambao ndio utakuwa na maamuzi ya mwisho
ya kuamua ni kiongozi gani mwenye nia ya dhati katika kukifanya Chama cha
Mapinduzi kuendelea kuongoza.
Alisema iwapo wajumbe wa mkutano wa
uchaguzi watamuamini kama ambavyo ameaminiwa na vikao vya juu vya Chama
atahakikisha anaondoa dhana ya makundi yaliyokuwa yamejengwa na viongozi wenye
kupenda ubinafsi badala ya kuwaunganisha wanachama na kufanya kazi za Chama
Sanya alisema ni muhimu kutolewa kwa elimu ya Chama kwa Wanachama ili
kila mmoja aweze kuelewa umuhimu wake ndani ya Chama na kutekeleza majukumu
yanayompasa katika kukitumikia na kujitambua.
Alisema wapo wagombea ambao wanaomba nafasi kwa ajili ya kutafuta majina na umaarufu na kushindwa kuzitumia kwa kuleta ufanisi na mabadiliko ndani ya Chama hicho na kufanya kuyumba kwa Wanachama huku wengine wakikimbilia katika vyama vya upinzani.
Aliongeza kuwa ni vyema Mwanachama unapoomba nafasi ya uongozi kujiuliza nini utakifanyia Chama kuliko kuomba nafasi kwa kutafuta ufahamike na kuhudhuria vikao bila kuwa na mipango ya kujua namna ya kuongeza Wanachama na kuwajenga kiimani Wanachama wote ili kuepuka mkanganyiko.
Alisema ni muhimu kuendesha madarasa ya itikadi ili kuwafanya wanachama na viongozi wao kujua kwa nini akawa kiongozi ama mwachama kwa kufanya hivyo kila mwanachama atajitambua na kuwa na ujasili binafsi badala ya kusubiri asemewe kila wakati na kupoteza haki zake kichama.

Akizungumzia masuala ya kiuchumi
Sanya alisema kutokana na vitega uchumi vilivyopo ndani ya Chama hicho
ataanzisha makampuni ya biashara ya ushindani kila Wilaya ya Mkoa wa Mara ili
kila kada wa Chama hicho aweze kujipatia kipato na kuendesha maisha pamoja na
kufanya kazi za Chama.
Alidai kutokana na vitega uchumi hivyo atahakikisha anasimamia akiwa
kama mwana uchumi ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi ndani ya Chama cha
Mapinduzi na kila mmoja aweze kuvutiwa na Chama hicho si kwa sera peke yake
bali na kujiendesha kiuchumi.
Post a Comment
0 comments