0
     -WASUSIA KUANDIKA HABARI ZA POLISI

 Na Shomari Binda
         Musoma,

Licha ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi kuandamana kulaani mauaji ya kinyama ya Mwaandishi wa Habari wa kituo cha televisheni cha Channel ten Daudi Mwangosi Waandishi wa Habari Mkoani Mara wameamua kuandamana kulaani kitendo hicho.

Mapema majira ya saa moja asubuhi katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mara (MRPC) Waandishi kutoka Wilaya za Mkoa huo walianza kuwasilia kwa ajili ya kutekeleza suala la kuandamana kulaani maauji hayo ya kinyama kwa Mwaandishi huyo wa Habario wa Mkoani Iringa.

Waandishi wakiwa katika mnaandalizi ya kuanza maandamano hayo majira ya saa mmbili na nusu alifika katika ofisi hizo OC CID wa Wilaya ya Musoma Mahamudi Banga kwa niaba ya Mkuu wa Polisi ya Wilaya ya Musoma akiwa na barua yenye kumbukumbu MUS/A.3/VOL 11/.378 ikitaka kuzuia maandamano hayo kwa kwa kile kilichoelezwa katika barua hiyo kuvunja kifungu namba 43(1)ya Polisi na wasaidizi Polisi 2002 ya kutoa taarifa kwa masaa 48.

Ktokana na katazo hilo na unyeti wa suala la maandamano hayo ambayo yalikuwa ya amani,Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mara Emanuel Bwimbo alishinikiza kufanyika kwa maandamano hayo na kukabiliana kwa chochote ambacho kingetokea.

Katika maandamano yaliayoanza majira ya saa tano asubuhi Waandishi wa Habari Mkoani Mara wakiwa na mabango yanayolaani tukio hilo walipitia katika barabara za kusaga-Nyerere kupitia NMB na kurudi katika ofisi za chama hicho zilizoo katika jengo la Bodi ya pamba.

Baada ya maandamano hayo Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mara alitoa tamko la kulaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mkoani Mara kuzuia maandamano hayo na kitendo cha mauaji ya Mwaandishi wa Habari akiwa kazini na kutangaza kususia kuandika Habari za Polisi hadi pale watakapoona umuhimu wa suala la mauaji hayo.

"Nawatangazia Waandishi wa Habari Mkoani Mara kuacha kuandika habari za Jeshi la Polisi mpaka pale watakapoona umuhimu wa suala hili na umuhimu wa vyombo vya Habari na yeyote atakayekiuka tutamtenga na kumfutia uanachama akafanye kazi za Jeshi la Polisi"alisema Bwimbo.

Alisema Jeshi la Polisi limekuwa likivitumia vyombo vya habari kutaka kupata umaarufu pale wanapokamata bangi na mambo mengine ya kiualifu na kupanda vyeo lakini wamekuwa hawatahamini vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari.

Bwimbo alidai Serikali inapaswa kutoa tamko kuhusu Uhuru wa vyombo vya Habari na itambue umuhimu wa vyombo vya Habari na kubadili mfumo wa utendaji wa Jeshi la Polisi ili kuweza kukomesha mauaji yasiyo na hatia kwa Wananchi wa Tanzania.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mara amewataka Waandishi wote Tanzania kuacha kuandika Habari za Jeshi la Polisi hadi pale yatakapotolewa matamko sahii kuhusiana na kifo cha Mwaandishi wa Habari Daudi Mwangosi.

Post a Comment