0
 HII ILIKUWA SIKU YA UZINDUZI WA MASHINDANO YA KOMBE LA POLISI JAMII KANDA MAALUMU YA TARIME RORYA,KATIBU TAWALA WA WILAYA YA TARIME AKIKAGUA KIKOSI CHA TIMU YA MAFUNDI FC AMBAYO IMEFANIKIWA KUTINGA HATUA YA FAINALI ITAKAYOPIGWA SEPTEMBA 6 DHIDI YA HOME BOYS YA SIRARI


 JUMLA YA TIMU NANE ZILISHIRIKI NA KILA TIMU ILIPOKUWA IKITOLEWA KATIKA MASHINDANO HUKABIDHIWA SETI YA JEZI NA MPIRA

HUSIA NA MUHIMU KABLA YA MCHEZO

KAMANDA KAMUGISHA AKIWA NA ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN JIMBO LA TARIME

TIMU YA MAFUNDI FC WAKIWASALIMA WACHEZAJI WA TIMU YA SHIRATI FC KATIKA MCHEZO WA UFUNGUZI AMBAPO WALIIBUKA NA USHINDI WA MABAO MATATU KWA NUNGE.



Timu ya soka ya Mafundi fc ya Tarime na Home Boys ya Sirari kesho zitatoana jasho katika fainali ya kobe la Polisi Jamii Kanda maalumu ya Tarime Rorya itakayopigwa katika uwanja wa sabasaba Wilayani Tarime.

Akizungumza na Blogu hii kutoka Wilayani Tarime mmoja wa mratibu wa mashindano hayo Ahmed Feruz amesema maandalizi ya fainali hiyo yamekwisha kukamilika na kinachosubiliwa ni kufika kwa muda wa mchezo huo ambao unasubiliwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka katika Wilaya hiyo.

Feluz amesema kuwa timu ya Mafundi fc imefanikiwa kutinga hatua hiyo ya fainali kwa kuiondosha timu ngumu ya Tarime stars kwa stahili ya mikwaju ya penati 5-4 baada ya timu hizo kutoshana nguvu ya bila kufungana katika dakika 90 za mchezo wa nusu fainali ya kwanza.

Nusu fainali ya pili timu ya Home Boys fc almaarufu kama vijana wa Sagara walitinga fainali hiyo kwa kuiondosha timu ya Shirati fc baada ya kuitandika mabao 2-0 katika mchezo uliokuwa na ushindani takribani dakika zote za mchezo huo.

Kabla ya kufanyika kwa fainali hiyo itatanguliwa na sherehe za POLISI DAY zitakazoaanza majira ya saa 6 mchana katika viwanja vya Polisi Tarime ambapo askari na wadau mbalimbali wa Jeshi la Polisi watatunukiwa vyeti vya utendaji bora wa majukumu ya kulinda amani.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa ambapo Wananchi wa Wilayani Tarime/Rorya na maeneo jirani wameombwa kuhudhulia katika sherehe hizo ambazo zitapambwa na burudani mbalimbali za vikundi vya sanaa.

Post a Comment